Pata taarifa kuu
Michezo

Timu ya taifa ya Burundi Intamba mu Rugamba uso kwa uso kesho na Amavubi ya Rwanda katika mechi ya kirafiki

Maandalizi ya mechi ya kirafiki kati ya timu ya taifa ya Burundi Intamba Murrugamba na Amavubi ya Rwanda yanaendelea vema ambapo kesho March 5 timu hizo zitachuano katika uwanja wa mwanamfalme Louis Rwagasore Jijini Bujumbura. Timu zote mbili zimekuwa zikifanya mazoezi katika uwanja huo kwa nyakati tofauti.

Vijana wa Intamba mu rugamba wakifuata kwa makini ushauri wa kocha msaidizi
Vijana wa Intamba mu rugamba wakifuata kwa makini ushauri wa kocha msaidizi Amidou Hassan
Matangazo ya kibiashara

Vijana wa Amavubi kutoka nchini Rwanda tayari wapo jijini Bujumbura kwa ajili ya mechi hiyo muhimu ya kirafiki kati ya mataifa hayo jirani.

Timu ya taifa ya Burundi imewashusha vijana wake wanaochezea soka ya kulipwa katika mataifa mbalimbali duniani ambao wapo Bujumbura kwa ajili ya mpambano huo wa kirafiki na tayari wanafanya mazoezi kwa pamoja kwa ajili ya mechi hiyo.

Miongoni wa wachezaji wa burundi wanaokipiga ugenini ni pamoja na Amisi Cedric anayechezea Rayons Sports ya nchini Rwanda, Ntibazonkiza Saido anaye cheza soka ya kulipwa nchini Pologne, Papy Faty anaekipiga nchini Afrika Kusini, pamoja na Valerie Nahayo anaecheze soka ya kulipwa nchini Ubelgiji na Amisi Tambwe anaechezea klabu ya Simba nchini Tanzania.

Viongozi wapya wa shirikisho la soka nchini Burundi, wanapania kurejesha hadhi na ladhaa ya mpira wa miguu nchini Burundi iliotoweka katika miaka ya hivi karibuni.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.