Pata taarifa kuu
SOKA

Kilimanjaro Stars yaifungisha virago Uganda Cranes kombe la Chalenji

Bingwa mtetezi wa kombe la Challenji, Uganda Cranes ,jana Jumamosi wamefungishwa virago kurudi kwao Kampala na timu ya Tanzania bara Kilimanjaro Stars , kwa mikwaju mitatu ya penalti dhidi ya miwili baada ya kutoka sare ya magoli 2-2 katika dakika 90 za mchezo.

Kikosi cha Kilimanjaro Stars
Kikosi cha Kilimanjaro Stars rfikiswahili
Matangazo ya kibiashara

Mrisho Ngasa aliipa Tanzania ushindi wa magoli mawili katika muda wa kawaida wa mchezo wakati Daniel Sserunkuma na Martin Mpuuga , wakitikisa nyavu kwa upande wa Uganda na kuiwezesha timu hiyo nayo kupata ushindi wa magoli mawili.

Hata hivyo baada ya dakika 90 zilizoshindwa kuamua mshindi, mwamuzi wa Somalia Wish Yabarow alipuliza kipenga ishara ya kutamatisha mchezo huo lakini ikiwa ni isahara ya maandalizi kwa ajili ya mikwaju ya Penalti.

Daniel Sserunkuma ndiye aliyezamisha kabisa jahazi la Uganda Cranes baada ya Godfrey Walusimbi na Khalid Aucho kukosa Penalty huku Emmanuel Okwi na Hamis Kiiza wakiifungia Uganda mikwaju miwili ya penalti.

Kwa Upande wa Tanzania Erasto Nyoni na Mbwana Samata ndio walioksa penalti huku Amir Kiemba ,Patrick Yondani na Athuman Iddi wakifanikiwa kucheka na nyavu na hivyo kuipa Kilimanjaro Stars ushindi wa mikwaju 3-2

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.