Pata taarifa kuu
Burudani

Mcheza dansi wa Balee nchini Urusi Pavel Dmitrichenko kuhukumiwa kifungo cha miaka 9 jela kwa kummwagia tindikali mkurugenzi wa sanaa za jukwaani

Waendesha mashitaka nchini Urusi huenda wakamhukumu kifungo cha miaka 9 jela mcheza dansi wa Balee Pavel Dmitrichenko kwa tuhuma za kummwagia tindikali mkurugenzi wa sanaa nchini humo .

Mcheza dansi ya balee Pavel Dmitrichenko
Mcheza dansi ya balee Pavel Dmitrichenko theguardian.com
Matangazo ya kibiashara

Tukio hilo ambalo lilitekelezwa mnamo mwezi Januari mwaka huu kidogo limpofue macho mkurugenzi huyo kwa mujibu wa taasisi za Urusi.

Upande wa mashitaka pia umeitaka mahakama kumhukumu Yury Zarutsky anayeshukiwa kuwa mshirika wa Dmitrichenko kifungo cha miaka 10 jela kwa kummwagia tindikali usoni Sergei Filin.

Uhalifu huo wakutisha ulitikisa ulimwengu wa sanaa ya dansi nchini Urusi na kutia doa historia ya michezo hiyo ya jukwaani.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.