Pata taarifa kuu
MECHI ZA KUFUZU KOMBE LA DUNIA 2014

Uruguay yaiadhibu Jordan huku Mexico ikiweka matumaini yake hai baada ya kuifunga New Zeleand

Mechi za kuwania kufuzu kucheza fainali za kombe la dunia hapo mwakani nchini Brazil zimeendelea hiyo jana huku Uruguay wakichomoza na ushindi dhidi ya Jordan, wakati Mexico wakiendelea kufufua matumaini yao baada ya kuibuka na ushindi dhidi ya New Zeleand.

Moja ya goli lililofungwa na Mexico dhidi ya New Zeleand
Moja ya goli lililofungwa na Mexico dhidi ya New Zeleand Reuters
Matangazo ya kibiashara

Mechi hizo za mabara hatua ya mtoano zimechezwa hiyo jana kwenye viwanja viwili tofauti ambapo nchini Jordan, timu ya taifa ya nchi hiyo ilikuwa na kibarua dhidi ya Uruguay kwenye mchezo ambao, Uruguay waliibuka na ushindi.

Kwenye mechi hiyo ya mzunguko wa kwanza uliishuhudia timu ya taifa ya Uruguay wakiishushia kipigo cha mbwa mwizi timu ya taifa ya Jordan kwa kuitandika kwa mabao 5-0 kwenye mchezo uliotawaliwa na Uruguay.

Magoli ya Uruguay yalifungwa na Maximiliano Pereira katika dakika ya 22, huku bao la pili likifungwa na Cristian Stuani katika dakika ya 42 ya mchezo, bao la tatu lilifungwa na Nicolas Lodeiro huku la nne likifungwa na Cristian Rodriguez na lile lililohitimisha karamu ya magoli likifungwa na Edinson Cavani katika dakika ya 90.

Katika mechi nyingine timu ya taifa ya Mexico ilifanikiwa kuchomoza na ushindi wa mabao 5-1 dhidi ya New Zeleand kwenye mchezo ambao ni wazi sasa unaipa nafasi kubwa Mexico kuweza kusonga mbele.

Magoli ya Mexico yamefungwa na Paul Aguilar, Raul Jimenez, Oribe Peralta aliyefunga mawili na lile la mwisho likifungwa na Rafael Marquez, huku lile la kufutia machozi la New Zeleand likifungwa na Chris James.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.