Pata taarifa kuu
RIADHA-KENYA

Kenya yaonywa na Shirika la Kimataifa la kupambana na dawa zilizopigwa marufuku

Kenya huenda ikafungiwa na Shirika la Kimataifa linalopambana na matumizi ya dawa za kusimumua misuli dhidi ya wachezaji baada ya kushindwa kufanya uchunguzi na kutoa ripoti dhidi ya wanariadha wake.

Matangazo ya kibiashara

Shirika hilo la WADA linasema kuwa wanariadha 17 kutoka nchini Kenya tangu mwaka mwezi Januari mwaka 2012 wamefungiwa nje ya mashindano mbalimbali baada ya kubainika kuwa walitumia dawa za kusisimua misuli zilizopigwa marufuku ikilinganishwa na wawili tu ambao walibainika kati ya mwaka 2010 na 2012.

Onyo hilo la WADA kwa Kenya litajadiliwa mwezi ujao katika Mkutano wa Kimataifa wa washikadau wa shirika hilo utakaofanyika jijini Johannesburg nchini Afrika Kusini.

Licha ya Shirika hilo kutokuwa na mamlaka ya kuizuia Kenya kushiriki katika mashindano mbalimbali ya Kimataifa, ina uwezo wa kusema kuwa nchi hiyo imekuwa haishirikiani na Shirika hilo kutatua tatizo hili ambalo limeendelea kushuhudiwa kote duniani miongoni mwa wachezaji.

Hatua ya kuwafungia wanariadha wa Kenya inaweza kutolewa tu na Kamati ya Kimataifa ya Olimpiki, kuwazua wanaridha hao kushiriki katika mashindano yajayo ya Olimpiki.

Ripoti kutoka Shirika hilo inasema kuwa ziliipa Kamati ya Olimpiki ya Kenya hadi mwezi Novemba mwaka huu kuwasilisha ripoti yake lakini inavyoonekana hakuna kilichofanyika wakati huu zikisalia wiki mbili kuanza kwa kongamano hilo la kimataifa nchini Afrika Kusini.

Mwezi Oktoba mwaka uliopita, uchunguzi uliofanywa na runinga moja ya Ujerumani  ilidai kuwa kuna baadhi ya Madaktari nchini Kenya waliokuwa wanawapa wanariadha dawa zilizopigwa marufuku kuwasaidia kushinda mashindano mbalimbali tuhma ambazo Chama cha riadha nchini humo kimekanusha.

Mapema mwaka huu, Shirikisho la Kimataifa la Riadha IAAF lilituma wawakilishi wake nchini Kenya kuwafanyia uchunguzi wanaridha 40 kubaini ikiwa walitumia dawa za kusisimua misuli au la katika mashindano mbalimbali.

Ikiwa itabainika kuwa wanaridha hao walitumia dawa hizo watapokonywa mataji waliyoshinda katika mashindano mbalimbali duniani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.