Pata taarifa kuu
MICHEZO

Sepp Blatter akosoa majina mabaya anayopewa na vyombo vya habari kutokana na kashfa ya rushwa

Rais wa shirikisho la soka duniani FIFA Sepp Blatter amejibu madai dhidi yake kuhusu kashafa ya rushwa ambapo amesema kuwa yeye si kupe anyonyaye damu za watu kupitia soka na kuongeza kuwa faida ambayo shirika lake inazipata hugawanywa na kutumika katika michezo mbalimbali ya kimataifa. 

Rais wa shirikisho la soka duniano FIFA Sepp Blatter
Rais wa shirikisho la soka duniano FIFA Sepp Blatter REUTERS/Arnd Wiegmann
Matangazo ya kibiashara

Blatter ambaye amekuwa akikosolewa hadharani na vyombo vya habari katika miaka ya karibuni kufuatia madai makubwa ya rushwa katika taasisi hiyo kubwa ya soka duniani, alitoa hotuba ya kujisafisha wakati akihutubia jamii ya wanafunzi wa Umoja wa Oxford, kaskazini mwa London.

Aidha amesema kuwa vyombo vya habari vimempa majina ya kila namna ambayo kwa hakika yanaumiza na amekuwa akijiuliza ni kwa nini na amefanya nini hadi kufikia katika hali hiyo.

Blatter ambaye amekuwa rais wa FIFA tangu mwaka 2008 na kuongezewa miaka mingine minne mwaka 2011, hata hivyo amekiri kuwa yeye pamoja na FIFA wanahitaji kuboresha sifa zao.

Amesema watajitahidi kutazama namna bora ya kufanya shighuli zao na kuhakikisha wanajenga misingi imara ya dhidi ya maovu na uendeshwaji duni wa shughui za kibiashara.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.