Pata taarifa kuu
TENNIS

Federer abanduliwa nje ya michuano ya Shanghai Open

Mchezaji wa Kimataifa wa mchezo wa Tennis kwa upande wa wanaume Roger Federer anayeorodheshwa wa tano duniani, amebanduliwa nje ya michuano ya Kimataifa ya Shanghai Open  baada ya kufungwa na Mfaransa Gael Monfils kwa seti za 6-4 6-7(5) 6-3.

Matangazo ya kibiashara

Baada ya kushindwa katika seti ya kwanza, Federer ambaye ameshinda mataji 17 ya Kimataifa alionekana  kusuasua katika seti ya pili baada ya kupoteza kwa seti 3-5 kabla ya kufanikiwa kushinda seti ya nne.

Monfils sasa atamenyana na Novak Djokovic au Fabio Fognini katika hatua ya robo fainali ya michuano hiyo.

Siku ya Jumatano, bingwa mtetezi Novak Djokovic licha ya kuwa na jeraha alilopata wakati akiwa uwanjani alifanikiwa kumshindi Mhispania Marcel Granollers kwa seti za 6-2, 6-0 na kufuzu katika hatua ya robo fainali.

Mwargentina Juan Martin del Potro naye amefika katika hatua ya robo fainali baada ya Mjerumani Tommy Haas kujiondoa katika mzunguko wa mwisho wa michuano hiyo.

Del Porto sasa atamenyana na Mhispania Nicolas Almagro au Thomas Berdych wa Jamhuri ya Czech.

Wachezaji wengine ambao pia wamefuzu katika hatua ya robo fainali ni pamoja  na Novak Djokovic, Rafael Nadal na David Ferrer.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.