Pata taarifa kuu
SOKA-UGANDA-MOROCCO

Mechi ya kufuzu kwa kombe la dunia kati ya Uganda Cranes na Senegal kufanyika Morocco

Mchuano wa kufuzu kwa fainali za kombe la dunia za mwaka 2014 kati ya Senegal na Uganda unatarajiwa kupigwa nchini Morocco tarehe 7 ya mwezi Septemba mwaka huu. Kwa mujibu wa taarifa iliyochapishwa katika tovuti ya Shirikisho la soka duniani FIFA, mechi hiyo itafanyika katika mji mkuu wa Morocco, Marrakesh.

Matangazo ya kibiashara

Mataifa hayo yapo katika kundi J, na Senegal wanaongoza kundi hilo wakiwa na alama tisa,ikiwa ni alama moja mbele ya Uganda wenye pointi nane.

Senegal walizuiliwa kucheza katika viwanja vya nyumbani baada ya ghasia zilizozuka wakati wa mechi ya kufuzu kwa michuano ya AFCON ya mwaka 2013 dhidi ya Ivory Coast.

Uganda wanahitaji ushindi katika mechi hiyo ili waweze kuingia katika raundi ya mwisho ya michuano ya kufuzu kwa timu za Afrika kabla ya kuelekea Brazili hapo mwakani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.