Pata taarifa kuu
PARIS

Tour de France kuandaliwa nchini Uingereza mwaka 2014

Mji wa Leeds utakuwa mwenyeji wa awamu ya kwanza ya mashindano ya kimataifa ya kila mwaka ya kuendesha baiskeli ya Tour de France mwaka 2014.

Matangazo ya kibiashara

Baadaye mashindano hayo yatahamia katika eneo la Yorkshire kati ya tarehe 5 na 6 mwezi wa Julai kabla ya kukamilika kwa awamu ya tatu ya mashindano hayo jijini London.

Mara ya mwisho kabisa kwa mashindano hayo ya Tour de France kufanyika nchini Uingereza ilikuwa mwaka 2007 na kuvutia mashabiki zaidi ya Milioni mbili.

Mji wa Yorkshire ulishinda miji mingine kama Florence na Edinburgh ambayo pia ilitaka kuandaa mashindano hayo.

Mwaka 1974 na 1994 pia mashindano hayo yaliandaliwa nchini humo na kuvutia wapenzi wengi wa mchezo huo na itakuwa mara ya nnne kwa mashindano hayo kuandaliwa nchini Uingereza.

Waandalizi wa mashindano haya ya  kila mwaka wanasema watatoa maelezo zaidi kuhusu mashindano hayo mwezi wa Januari mwaka ujao jijini Paris Ufaransa.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.