Pata taarifa kuu
MICHEZO-CAF

Raisi wa Shirikisho la kandanda barani Afrika CAF Issa Hayatou kutua Kampala alhamisi

Raisi wa Shirikisho la kandanda barani Afrika CAF Issa Hayatou anatarajia kuwasili jijini Kampala nchini Uganda alhamisi juma hili wakati huu kuelekea kwenye michuano ya CECAFA inayoanza kutimua vumbi mwishoni mwa juma hili.

Raisi wa Shirikisho la kandanda barani Afrika,Issah Hayatou anataraji kutua jijini Kampala alhamisi juma hili
Raisi wa Shirikisho la kandanda barani Afrika,Issah Hayatou anataraji kutua jijini Kampala alhamisi juma hili mtnfootball.com
Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa Shirikisho la kandanda nchini Uganda FUFA, Hayatou atawasili sambamba na maafisa wengine wa CAF akiwemo Katibu Mkuu Hicham El Amrani.

Akiwa nchini Uganda Rais Hayatou atahudhuria mkutano wa CECAFA unaotarajiwa kufanyika katika hoteli ya Serena siku ya ijumaa juma hili kabla ya kuzinduliwa rasmi kwa michuano siku ya jumamosi katika uwanja wa Namboole.

Hayatou pia anatarajia kufanya mazungumzo na waziri wa michezo wa Uganda Charles Bakabulindi kabla ya kukamilisha ziara yake nchini humo.

Katika mechi ya ufunguzi siku ya jumamosi mabingwa watetezi wa kombe hilo Uganda wataumana na Kenya wakiwa wanawania kutwaa ubingwa wa kombe hilo kwa mara ya kumi na tatu.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.