Pata taarifa kuu
Kenya

Gor Mahia yaitandika 2-1 FC Leopards

Hatimaye ule mtanange wa Ligi kuu ya Tusker nchini Kenya uliokuwa ukingojewa kwa hamu baina ya watani wa jadi FC Leopards na Gor Mahia, umemalizika hapo jana katika dimba la MISC Kasarani huku FC Leopards ikikubali kichapo cha magoli 2-1. 

mechi kati ya Gor Mahia na FC Leopards kisarani Kenya
mechi kati ya Gor Mahia na FC Leopards kisarani Kenya afcleopards.blogspot.com
Matangazo ya kibiashara

Mtanange huo ambao uliwakutanisha mashabiki wa pande zote mbili waliofurika katika dimba la kasarani ulianza kwa timu ya Gor Mahia kumudu vema mpira kwa kipindi chote cha kwanza huku mshambuliaji Dan Serenkuma akifanikiwa kufunga magoli mawili katika kipindi hicho na kutimiza idadi ya magoli 12 katika ligi hiyo haadi sasa.

Katika kipindi cha pili vijana wa FC Leopards walizinduka kutoka usingizini na kufanikiwa kurejesha goli moja huku wakikosa magoli mengi katika kipindi cha pili.

Hadi mpira unamalizika, Gormahia waliendelea kusalia na magoli mawili ya ushindi huku FC Leopards wakiambulia goli moja na kukubali matokeo jambo lililosababisha mchezo huo kumalizika kwa amani.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.