Pata taarifa kuu
mochezo

Kiungo Luka Modric atua Real Madrid akitokea Tottenham

Kiungo Luka Modric amehama rasmi klabu aliyokuwa akisakata kabumbu Tottenham na kuanza mbio mpya katika kikosi cha Real Madrid kwa gharama za kitita cha yuro milioni 30.

Kiungo mchezaji Luka Modric,tayari ameingia mkataba kuchezea Real Madrid
Kiungo mchezaji Luka Modric,tayari ameingia mkataba kuchezea Real Madrid AFP
Matangazo ya kibiashara

Kiungo huyo raia wa Croatia mwenye umri wa miaka 26, alifanyiwa uchunguzi wa kiafya mapema jumatatu kabla ya kuingia mkataba wa miaka mitano na klabu kubwa ya Uhispania,Real Madrid.

Mchezaji huyo amefurahi na kueleza kuwa ni heshima kubwa kwake kujiunga katika klabu kubwa na bora ulimwenguni.

Nayo klabu ya Tottenham haikukaa kimya ilitangaza kuingia ushirika na klabu hiyo ya Real Madrid ambapo klabu hizo mbili zitashirikiana kwa maana ya wachezaji wao,makocha na mahusiano ya kibiashara.

Naye Mwenyekiti wa Tottenham Daniel Levy amesema kuwa Luka ni mchezaji makini ambaye wasingependa aondoke klabuni lakini inatia faraja kuona atachezea Real Madrid,klabu ambayo Tottenham inamatarajio makubwa ya kushirikiana kwa manufaa ya klabu hizo.

Modric alijunga Tottenham mwaka 2008 kwa gharama za yuro milioni 16.5 na kucheza mechi lukuki jijini London na kufunga magoli 17.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.