Pata taarifa kuu
LONDON-OLYMPICS 2012

Algeria yapata medali kwenye mbio za mita 1500, leo ni zamu ya Caster Semenya wa Afrika Kusini kwenye mita 800

Mwanariadha wa Algeria, Taoufik Makhloufi amefanikiwa kutwa amedali yake ya kwanza ya dhahabu hapo jana usiku baada ya kufanikiwa kushinda mbio za mita 1500 na kutengeneza historia yake. 

Mwanaridaha wa Algeria, Taoufik Makhloufi akishangilia mara baada ya kushinda mbio za mita 1500
Mwanaridaha wa Algeria, Taoufik Makhloufi akishangilia mara baada ya kushinda mbio za mita 1500 Reuters
Matangazo ya kibiashara

Makhloufi mwenye umri wa maiaka 24 alimaliza mbio hizo kwa kutumia muda wa dakika tatu na sekunde 34.08 akifuatiwa na Mmarekani Leonel Manzano na Mmorocco, Abdalaati.

Kwenye mashindano hayo wakiambiaji wa Kenya ambao walipewa nafasi kubwa ya kuweza kufanya vyema kwenye mbio hizo walishindwa kufua dafu baada ya mwanariadha wake Silas Kiplagat kumaliza kwenye nafasi ya 7.

Hii leo kutakuwa na mbio nyingine ambapo mwanariadha toka Afrika Kusini anayeshikiliwa rekodi ya dunia ya mita 800 Caster Semenya anatarajiwa kurejea tena kwenye mbio hizo baada ya kuwa nje ya uwanja kwa kipindi kirefu.

Mwanariadha wa Jamaica Usain Bolt yeye anatarajiwa kushiriki nusu fainali ya mbio za mita 200 kwa upande wa wanaume kwenye mbio ambazo zinatarajiwa kuvuta hisia za mashabiki wengi wa mchezo huo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.