Pata taarifa kuu
TANZANIA

Yanga yang'ara tena kombe la Kagame

Hatimaye timu ya Young Africans( Yanga ) ya Dar es Salaam nchini Tanzania imefanikiwa kutea ubingwa wake na kutwaa kombe la Kagame kwa mara ya pili mfululizo baada ya kuipa kichapo cha magoli 2 -0 timu ya soka ya Azam FC ambayo imeshiriki mashindano hayo kwa mara ya kwanza. 

Wachezaji wa Yanga wakifurahia ushindi
Wachezaji wa Yanga wakifurahia ushindi michuzijr2.wordpress.com
Matangazo ya kibiashara

Yanga ambao hata hivyo hawakuanza vizuri mchezo huo hapo jana huku wapinzani wao wakionekana kupania zaidi kupata ushindi hata hivyo waliweza kupenya nyavu za Azam FC katika dakika ya 44 ya kipindi cha kwanza goli lilofungwa na Hamis Kiiza.

Katika kipindi cha pili Yanga walijipanga vema na kuonesha mashambulizi na hatimaye katika dakika ya tatu ya muda wa nyongeza katika kipindi cha pili mchezaji Said Bahanuzi alikamilissha safari ya ushindi ya klabu ya Yanga.

Kwa matokeo hayo Yanga sasa imetawazwa rasmi kuwa mshindi wa kombe la Kagame na kufikisha rekodi ya mara tano ya kutwaa kombe hilo ambapo walitwaa kombe hilo mwaka 1975, 1993, 1999, 2011 na 2012.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.