Pata taarifa kuu
Michuano ya Francophonie Dar Es Salaam

Timu ya Kampuni ya Total yatwaa ubingwa wa michuano ya Francophonie jijini Dar Es Salaam

Timu ya soka ya kampuni ya mafuta Total imetwaa kombe la michuano ya Francohonie, iliofanyika jana jijini Dar Es Salaam nchini Tanzania. Michuano hiyo ilijumuisha timu kumi na mbili zilizo gawika katika makundi matatu, huku kila kundi ikiwa na timu nne.

Captaine wa timu ya Total akikabidhiwa kombe la Francophonie msimu wa 2012
Captaine wa timu ya Total akikabidhiwa kombe la Francophonie msimu wa 2012 RFI/BILALI
Matangazo ya kibiashara

Michuano hiyo ya Francophonie jijini Dar Es Salaam, ilizikutanisha timu ya Alliance Francaise ya Dar Es Salaam, timu ya chuo kikuu cha Dar Es Salaam, RFI, Canada, Ubalozi wa Ufaransa, Ubalozi wa Liban, Ubalozi wa DRCongo, timu ya Kampuni ya Total, timu ya benki ya Edvans, timu ya ubalozi wa Uswisi, Ecole Francaise ya Dar Es Salaam na TPS.

Baada ya mzunguuko wa kwanza na wapili, timu nne ndizo zilisalia kwenye nusu fainali, ambapo RFI ilikutana na Total na kujikuta ushindi unaiendea timu ya Total baada ya kuongezwa muda wa ziada, kwani timu hizo zilitoka sare ya kufungana bao moja kwa moja, huku kukiwa na lawama uapnde wa wachezaji wa RFI kuhusu muamuzi ambae alionekana kuegemea upande umoja.

Upande mwingine timu ya Alliance Francaise katika mechi yao ya nusu fainali, ilijikuta imelazimishwa matuta na timu ya Ubalozi wa DRCongo, na kutwaa ushindi huo wa matuta.

Fainali ilizikutanisha Alliance Francaise na Total. Timu hizi zilishindwa kufungana hadi muda wa ziada na kulazimishana matuta. Total ilitwaa kombe hilo kwa kuishinda Alliance Francaise kwa penalti ambapo wachezaji wawili wa Alliance Francaise walishindwa penalti mbili, hivyo Total ikapewa kombe hilo la Francophonie. Timu ya Ubalozi wa DRCongo ndio ilikuwa imechukuwa kombe hilo mwaka uliopita.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.