Pata taarifa kuu
UINGEREZA

Wenger atamba Arsenal kuanza kazi wakati Sir Ferguson akipongeza rekodi ya Giggs

Kocha Mkuu wa Arsenal Arsene Wenger ametamba timu yake imerejea tena kwa nguvu kitu ambacho kitafufua matumaini yao ya kuweza kuleta ushindani katika mbio za ubingwa mwaka huu.

Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger akiwa kwenye harakati za kutoa maelezo kwa wachezaji wake
Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger akiwa kwenye harakati za kutoa maelezo kwa wachezaji wake Reuters/Giorgio Benvenuti
Matangazo ya kibiashara

Matumaini ya Wenger yamekuja baada ya Arsenal kufanikiwa kutoka nyumba kwa magoli mawili na kisha kupata ushindi wa magoli 5-2 mbele ya Tottenham na kukwea hadi nafasi ya nne kwenye msimamo wa ligi.

Wenger amesema timu hiyo imefufua matumaini yake mapya tofauti kabisa na wengi ambavyo wamekuwa wakifikiri kuwa timu hiyo imepoteza mwelekeo katika kinyang'anyiro cha kusaka ubingwa wa msimu huu.

Tottenham kwenye mchezo wa jana walipata magoli yao kupitia kwa Louis Saha na Emmanuel Adebayor kabla ya Arsenal kuibuka kutoka kwenye ushindi na kufunga kupitia Bacary Sagna, Robin Van Persie, Tomas Rosicky na Theo Walcott ambaye alifunga magoli mawili.

Wenger pia amesifu kiwango ambacho kimeoneshwa na Walcott kwenye mchezo huo na kufanikiwa kufunga magoli mawili yaliyoisaidia Arsenal kurejea kwenye nafasi nne za juu kwenye msimamo.

Kwa upande wake Kocha Mkuu wa Manchester United Sir Alex Ferguson amesifu rekodi ya michezo mia tisa ambayo ameifikisha Ryan Giggs na kuisaidia timu yake kupata ushindi mbele ya Norwich City.

Sir Ferguson amesema kwa mchezaji kufikisha michezo mia tisa akiwa kwenye klabu moja ni kitu cha kipekee na kinachostahili kupongezwa kwa kiwango kikubwa sana na anakiri golio alilofunga dhidi ya Norwich alistahili.

Manchester United imefanikiwa kupata ushindi dhidi ya Norwich City kwa magoli 2-1 huku goli la kwanza likifungwa na mkongwe mwingine Paul Scholes na hivyoe kuendelea kukabiliana na wapinzani wao Manchester City kwenye mbio za ubingwa.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.