Pata taarifa kuu
Michezo, FIFA

FIFA yawasimamisha kazi Bin Hammam na Warner, na kumtakasa Blatter

Shirikisho la soka duniani FIFA, limewasimamisha kwa muda viongozi wake, Mohamed Bin Hammam kiongozi wa shirikisho la soka barani Asia na Jack Warner naibu rais wa FIFA kwa tuhuma za ufisadi.

Jack Warner akizungumza na waandishi habari kwenye hoteli moja mjini Zurich Mei 30,  2011.
Jack Warner akizungumza na waandishi habari kwenye hoteli moja mjini Zurich Mei 30, 2011. REUTERS/Arnd Wiegmann
Matangazo ya kibiashara

Uamuzi huo ulifikiwa jana jumapili baada ya mkutano wa kamati ya nidhamu na maandali, dhidi ya tuhUma kuwa Mohamed Bin Hammam, Jack Warner waliwahonga maafisa wa kandanda kutoka Carribean $ 40,000 wakati wa kampeni za Bin Hammam mapema mwezi huu.

Aidha, FIFA imewasimamisha kazi viongozi wa kandanda katika visiwa hivyo vya Carrebian Debbie Minguell na Jason Sylvester.

Mapema hapo jana Bin Hamman aliyekuwa ametangaza kuwania uenyekiti wa FIFA, alijiondoa katika kinyangayiro hicho, uchaguzi utakaondaliwa siku ya Jumatano kwa kile alichokisema kuwa, anataka kulinda jina la FIFA.

Hata hivyo,kamati hiyo ya maadili ilimwondolea tuhuma zozote za ufisadi rais Sep Blatter huku, katibu mkuu wa FIFA Jerome Valcke akisema kuwa uchaguzi wa Jumatano utaendelea kama ulivyopangwa.

Kamati hiyo ya FIFA imetangaza kuwa itaanzisha uchunguzi zaidi dhidi ya maafisa hao, ambao kwa sasa inasema hawana makosa na ikiwa watapatikana na makosa hayo ya ufisadi, wataondolewa kabisa katika shirikisho hilo na kupigwa marufuku kushiriki katika shughuli zozote za kandanda.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.