Pata taarifa kuu
YEMEN-USALAMA

Shambulio dhidi ya meli ya mafuta lazimwa Yemen

Muungano wa nchi za Kirabu unaoongozwa na Saudia, ambao umeingilia kijeshi nchini Yemen tangu mwaka 2015, umetangaza kwamba umezima shambulio lililokuwa limelenga meli ya mafuta kwenye Bahari ya Oman, shirika la habari la serikali ya Saudia la SPA limeripoti leo Jumatano.

Meli hiyo ilikuwa ikisafiri kwenye umbali wa maili 90 kusini mwa bandari ya Yemen ya Nishtun kuelekea Ghuba ya Aden wakati ilishambuliwa na meli nne.
Meli hiyo ilikuwa ikisafiri kwenye umbali wa maili 90 kusini mwa bandari ya Yemen ya Nishtun kuelekea Ghuba ya Aden wakati ilishambuliwa na meli nne. (Photo : AFP)
Matangazo ya kibiashara

Meli hiyo ilikuwa ikisafiri kwenye umbali wa maili 90 kusini mwa bandari ya Yemen ya Nishtun kuelekea Ghuba ya Aden wakati ilishambuliwa na meli nne, msemaji wa muungano wa nchi za Kiarabu, Turki al Malki, amesema katika taarifa kwa shirika la habari la serikali ya Saudi Arabia la SPA.

Taarifa hiyo haijataja chanzo cha shambulio hilo na haijatoa maelezo mengine kuhusu meli hiyo.

Saudi Arabia inaongoza muungano wa nchi za Ghuba zinazopambana kijeshi nchini Yemen dhidi ya waasi wa Kishia wa Houthi wanaoungwa mkono na Iran, ambao wamedhibiti miji mikubwa ya nchi hiyo tangu mwishoni mwa mwaka wa 2014.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.