Pata taarifa kuu
AFGHANISTANI-MAREKANI-USALAMA

Marekani yataka kuahirishwa kwa zoezi la kutawazwa rais wa Afghanistan Ashraf Ghani

Marekani inataka rais wa Afghanistan Ashraf Gahni kusogeza mbele sherehe ya kutawazwa kwake kwa muhula wa pili ili sherehe hiyo isihatarishi juhudi zake za amani nchini Afghanistan, shirika la Habari la Reuters limenukuu vyanzo viwili vilivyoarifiwa juu ya hoja hii.

Rais wa Afghanisatn, Ashraf Ghani (Julai 9, 2018).
Rais wa Afghanisatn, Ashraf Ghani (Julai 9, 2018). WAKIL KOHSAR / AFP
Matangazo ya kibiashara

Ashraf Ghani wiki iliyopita alidai alishinda uchaguzi wa urais uliyofanyika Septemba 28 na anatarajia kutawazwa Alhamisi wiki hii, afisa mmoja wa Afghanistan amesema.

Mpinzani wake, Abdullah Abdullah, pia alijitangaza mshindi wa uchaguzi huo na anataka kuandaa sherehe yake ya kutawazwa, vyombo vya habari vya Afghanistan vimeripoti.

Marekani mpaka sasa haijatambua mshindi wa uchaguzi wa urais nchini Afghanistan na hali hii inatishia mchakato wa amani, mchakato ambao unasimamiwa na Marekani. Mchakato huo uliingia katika hatua muhimu Jumamosi iliyopita pamoja na kuanza kwa kipindi cha utulivu baada ya makubaliano na Taliban, na kunatarajiwa Jumamosi ijayo, zoezi la kutia saini kwenye mkataba kati ya Washington na wapiganaji wa Kiisilamu wa Taliban kuhusu kuondoka kwa vikosi vya Marekani nchini Afghanistan.

Mkataba huo utafuatiwa na mazungumzo baina ya wadau katika mgogoro nchini Afghanistan kufikia suluhisho la kisiasa baada ya nchi hii kukumbwa na mgogoro kwa miongo kadhaa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.