Pata taarifa kuu
UTURUKI-URUSI-SYRIA-USALAMA

Syria: Ankara yatishia kuwashambulia wanajihadi Idleb

Uturuki imetangaza Alhamisi (Februari 13) kwamba itatuma vikosi vipya katika mji wa Idleb, kaskazini magharibi mwa Syria. Uturuki inatishia kwa mara ya kwanza kushambulia wanajihadi katika mji huo ikiwa hawataheshimu makubaliano ya kusitisha mapigano yanaotakiwa kumaliza vita katika jimbo hilo la waasi.

Askari wa jeshi la Uturuki katika mji wa Binnish Kaskazini Magharibi mwa Mkoa wa Idleb Februari 12, 2020.
Askari wa jeshi la Uturuki katika mji wa Binnish Kaskazini Magharibi mwa Mkoa wa Idleb Februari 12, 2020. Muhammad HAJ KADOUR / AFP
Matangazo ya kibiashara

Zoezi la kupeleka wanajeshi wa Uturuki katika mji wa Idleb litaendelea na sio tu, kama jinsi Ankara imekuwa ikisema kwa siku kadhaa, kuzuia vikosi vya utawala wa Bashar al-Assad kusonga mbele katika mkoa huu, au kuwarudisha nyuma mbali ya mipaka ya makubaliano ya Sochi yaliyofikiwa na Moscow mwaka 2018.

Waziri wa Ulinzi wa Uturuki Hulusi Akar amesema: "Kikosi kitatumika dhidi ya wale ambao hawaheshimu makubaliano ya kusitisha mapigano, pamoja na wale wenye itikadi kali. "

"Itikadi kali": maneneo yanayomaanisha wanajihadi wa kundi la Hayat Tahrir al-Cham, lenye uhusiano na Al-Qaeda, ambao kila wakati wamekuwa wakitengwa na makubaliano ya kusitisha mapigano. Lakini, chini ya maelewano ya Sochi, Uturuki ilikuwa imeamua kuwaondoa wanajihadi katika mkoa wa Idleb. Mpaka sasa, ilikuwa bado haijaweza kulitekeleza.

Jumatano wiki hii rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan alisema kwamba nchi yake itachukua hatua dhidi ya kundi la Hayat Tahrir al-Cham. "Kuanzia sasa, hatutopumbazwa tena [kwa] ushabiki, usaliti, uchochezi [...] kwa makundi ya upinzani ambayo hutoa kwa serikali kisingizio cha shambulio lake", Recep Tayyip Erdogan alitangaza.

Kubadilika kwa kauli kwa viongozi wa Uturuki ni ahadi ambayo Uturuki inatoa kwa Urusi ili kuishawishi kupata makubaliano ya kudumu huko Idleb.

Mapema Jumatano, wakati rais Recep Tayyip Erdogan alikuwa ameahidi kushambulia vikosi vya serikali ya Syria baada ya askari wa Uturuki kushambuliwa, Urusi - mshirika mkuu wa serikali ya Syria- ilikuwa imeishtumu Ankara kwamba haifanya chochote kwa "kuwaangamiza" magaidi huko Idleb ".

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.