Pata taarifa kuu
UTURUKI-MAREKANI-ISRAEL-PALESTINA-USALAMA

Mpango wa Trump kwa Mashariki ya Kati: Erdogan alaani "usaliti" wa baadhi ya nchi za Kiarabu

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan ameshtumu baadhi ya nchi za Kiarabu kwa kufanya "uhaini" kwa kukaa "kimya" kuhusu mpango wa Marekani ambao kulingana na rais wa nchi hiyo, Donald Trump, unalenga kumaliza mzozo kati ya Israeli na Palestina.

Rais wa Uturuki Tayyip Erdogan katika mkutano huko Ankara mnamo Januari 2, 2020.
Rais wa Uturuki Tayyip Erdogan katika mkutano huko Ankara mnamo Januari 2, 2020. Murat Cetinmuhurdar/Presidential Press Office/Handout/REUTERS
Matangazo ya kibiashara

"Nchi za Kiarabu ambazo zinaunga mkono mpango kama huo zinafanya usaliti kwa Jerusalem, na pia kwa raia wake, na zaidi, kwa binadamu wote," Erdogan amesema wakati wa hotuba mbele ya maafisa wa chama chake AKP, huko Ankara.

"Saudi Arabia imekaa kimya. Lini utaongea usikike? Oman, Bahrain, hali kadhalika. Serikali ya Abu Dhabi inakaribisha mpago kama huo. Hamna hata aibu! " Erdogan amesema katika hotuba yake Ankara.

Erdogan, anayedai kuwa ni mtetezi mkuu wa Palestina, alisema siku ya Jumatano kwamba mpango huo, ambao unaeleza kwamba Jerusalem ni "mji mkuu usiogawanyika wa Israel", ni jambo lisilokubalika kabisa.

"Uturuki haitambui na haikubali mpango huo ambao unaidhoifisha Palestina na kuitukuza Israel," Erdogan amesema leo Ijumaa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.