Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 25/02 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 25/02 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 24/02 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Mashariki ya Kati

Iran: Urushwaji wa makombora ni mwanzo wa kujilipiza kisasi

media Ayatollah Ali Khamenei ndiye kiongozi wa dini mbali na kuwa kiongozi mkuu wa utawala wa Iran. Yeye ndiye anayefanya uamuzi wa mwisho kuhusu msawala ya kisiasa nchini Iran,Tehran, Iran, Januari 8, 2020. Official Khamenei website/Handout via REUTERS

Hatua ya Iran kurusha makombora Jumatatu wiki hii dhidi ya kambi mbili za jeshi zinazotumiwa na askari wa Marekani nchini Iraq, haikuwa na lengo la kuua askari wa Marekani, bali kuharibu "mitambo ya jeshi" la Marekani, amesema afisa wa ngazi ya juu wa jeshi la walinzi wa mapinduzi.

Akinukuliwa na televisheni ya serikali ya Iran, Amir Ali Hajizadeh, mkuu wa kikosi cha anga cha pasdaran amesema hatua hiyo inaashiria mwanzo wa mfululizo wa mashambulizi katika ukanda huo wa Mashariki ya Kati.

Amir Ali Hajizadeh amesema "kuondoka kwa vikosi vya Marekani vilivyoko Mashariki ya Kati ni matunda ya ulipizaji kisasi baada ya kifo cha Jenerali Qassem Soleimani, aliyeuawa Ijumaa iliyopita katika shambulizi la anga la Marekani jijini Baghdad, nchini Iraq.

Afisa huyo amedai kwamba Tehran ilikuwa, kabla ya shambulio lake siku ya Jumatano, na lengo la "kushambulia mitambo ya mfumo mzima wa kuendesha na kuratibu ndege za kivita za Marekani na zile zisizo kuwa na rubaniwa".

Wakati huo huo Marekani imesema iko "tayari kujadiliana na Iran bila masharti" baada uhasama uliozuka baina ya nchi hizo kufuatia mauaji ya jenerali Qasim Soleimani.

Katika waraka wake kwa Umoja wa Mataifa, Marekani ilijitetea kuwa ilimuua jenerali wa jeshi la Iran Qasem Soleimani kama hatua ya kujilinda.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana