Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 25/02 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 25/02 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 24/02 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Mashariki ya Kati

Watu 170 wafariki dunia katika ajali ya ndege ya Ukraine Tehran

media Ndege ya Ukriane, Boeing373 yaanguka nchini Iran, takriban 170 wamefariki dunia. © AFP

Takribani watu 170 wamefariki dunia katika ajali ya ndege aina ya Boeing 373 ya shirika la ndege la Ukraine International Airlines. Ndege hiyo imeanguka nchini Iran leo Jumatano muda mfupi baada ya kupaa kutoka uwanja wa ndege wa kimataifa waTehran ikielekea Kiev, vyombo vya habari vya Iran vimeripoti.

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amethibitisha kuwa hakuna aliyenusurika katika ajali hiyo.

"Abiria wote na wafanyakazi" wa Boeing 737 ya shirika la ndege la Ukraine International Airlines "wamefariki dunia," Bw Zelensky ameandika kwenye ukurasa wake wa Facebook.

Muda mfupi kabla, afisa mwandamizi kwenye wizara ya Mambo ya Nje ya Ukrainewa, Vassyl Kyrylytch, amelithibitisha shirika la habari la AFP kwamba hakuna aliyenusurika katika jalai hiyo.

Amesema kuwa "kulingana na takwimu za awali, kulikuwa na watu 168 katika" ndege hiyo ambayo ilikuwa ikisafiri kutoka mji mkuu wa Iran kwenda Kiev.

"Hakuna matumaini yoyote ya kuwapata watu walionusurika katika ajali ya ndege hiyo PS-752 iliyokuwa ikisafiri kutoka Tehran kwenda Kiev," mkuu wa shirika la mwezi mwekundu, ISNA, Morteza Salimi amesema.

Ajali hiyo ilisababishwa na "matatizo ya kiufundi," Press TV imemnukuu Ali Khashani, msemaji wa mamlaka ya Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Imam Khomeiny, nchini Iran.

 

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana