Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 25/02 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 25/02 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 25/02 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Habari mpya kabisa
Mashariki ya Kati

Marekani yamnyima visa Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran

media Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Mohammad Javad Zarif, hapa ilikuwa Mei 8, 2019 huko Moscow. REUTERS/Evgenia Novozhenina

Marekani imekataa kutoa visa kwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Mohammad Javad Zarif, ambaye alitarajiwa kuhudhuria mkutano wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa jijini New York Alhamisi wiki hii, kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters likimnukuu afisa mmoja wa Marekani.

Taarifa hiyo ya afisaa huyo, ambaye hakutaja jina lake, inakwenda sanjari na ongezeko la mvutano kati ya Iran na Maekani baada yashambulio la Marekani nchini Iraq lililomuua Jenerali Qassem Soleimani usiku wa Alhamisi kuamkia Ijumaa wiki iliyopita.

Hali hii imeendelea kuzua hofu katika ukanda wa Mashariki ya Kati, ambapo hivi kar9buni baadhi ya raia wa Marekani walilaziumika kuondoka nchini Iraq na Iran.

Hivi karibuni Ufaransa, Ujerumani na Uingereza zilito wito kwa Iran na Maekani kusitisha mvutano unaoendelea, na kuitaka Iran kuheshimu mkataba wa mpango wa nyuklia uliofikiwa mnamo mwaka 2015.

Tehran iliahidi kulipiza kisasi kifo cha Jenerali Qassem Soleimani, aliyeuawa siku ya Alhamisi usiku katika shambulizi la anga la Marekani mjini Baghdad nchini Iraq.

Siku ya Jumapili Iran ilitangaza kwamba itajiondoa kwenye mpango wa nyuklia uliofikiwa mwaka 2015 na kwamba itakiuka kiwango cha urutibishaji wa madini ya Uranium kilichowekwa katika makubaliano ya nyuklia ya mnamo 2015 yalioidhinishwa na mataifa yenye nguvu duniani.

Uingereza, Ufaransa na Ujerumani zimeionya Iran dhidi ya hatua hiyo inayokwenda kinyume na makubaliano hayo.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana