Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 25/02 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 25/02 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 24/02 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Mashariki ya Kati

Arobaini wauawa katika mkanyagano Iran

media watu 35 wameripotiwa kufarika kufuatia kisa cha mkanyagano katika mazishi ya Qasem Soleimani, jenerali wa kikosi maalum cha jeshi la Iran alieuawa na Marekani wiki iliyopita. ATTA KENARE / AFP

Watu zaidi ya 40 wamepoteza maisha katika mji wa Kerman nchini Iran, baada ya kukanyangana wakati wa mazishi ya kiongozi wa kijeshi nchini humo Jenerali Qasem Soleimani, aliyeuawa wiki iliyopita baada ya kushambuliwa na ndege ya kivita ya Marekani nchini Iraq.

Maelfu ya waombolezaji walikuwa wamekusanyika katika mji huo wa Kerman alikozaliwa Jenerali huyo, kuhudhuria mazishi yake baada ya kifo hicho ambacho kimeleta huzuni mkubwa nchini Iran.

Maafisa wanasema kuwa watu wengine zaidi ya 190 walijeruhiwa katika mkanyagano huo wa watu waliokuja kutoa heshima zao za mwisho kwa Jenerali huyo waliyemwita shujaa.

Idadi kubwa ya waombolezaji ilisababisha wengine kukimbilia katika milima ya jirani katika mji huo, ili kufuatilia tukio hilo la mazishi.

Viongozi wa Iran wameendelea kuilaani Marekani na kusema kuwa kumuua kiongozi huyo wa kijeshi, wameipa nguvu ya kuendeleza harakati za kupambana na nchi hiyo.

Mauaji haya yamesabisha uhusiano mbaya kati ya Iran na Marekani, huku wabunge nchini Iran wakipitisha mswada na kuwaita wanajeshi wa Marekani magaidi.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana