Pata taarifa kuu
IRAN-MAREKANI-IRAQ-USALAMA

Iran waomboleza kifo cha Jenerali Soleimani

Ibada za kuomboleza kifo cha Qassem Soleimani na wenzake waliouawa wiki iliyopita katika shambulio la anga la Marekani mjini Baghdad nchini Iraq, zinaendelea, jijini Tehran.

Jeneza la Qassem Soleimani liliwasili nchini Iran jana Jumapili huko Ahvaz ambapo lilipokelewa na umati mkubwa wa watu.
Jeneza la Qassem Soleimani liliwasili nchini Iran jana Jumapili huko Ahvaz ambapo lilipokelewa na umati mkubwa wa watu. Hossein Mersadi/Fars news agency/WANA (West Asia News Agency) vi
Matangazo ya kibiashara

Jumatatu hii asubuhi watu wamefurika katika mwa mji wa Tehran, wakisubiri sala ya kuaga mwili wa jenerali wa ngazi ya juu wa jeshi la Iran Qassem Soleimani, mkuu wa operesheni za nje za Iran katika kikosi cha al-Quds cha Walinzi wa Mapinduzi, kinachoongozwa na kiongozi Mkuu wa Iran.

Umati wa watu umekusanyika mapema asubuhi kwenye uwanja maalumu, huku shrehe hiyo ikirushwa moja kwa moja kwenye televisheni na radio mbalimbali nchini Iran.

Jenerali Qassem Soleimani, aliuawa katika shambulio la Marekani mjini Baghdad nchini Iraq. Mauaji hayo yaliamrishwa na Rais Donald Trump, ambaye alisema kamanda huyo wa kikosi cha al-Quds cha jeshi la Ulinzi wa Mapinduzi la Iran, alikuwa anapanga mashambulizi dhidi ya wanadiplomasia na wanajeshi wa Marekani nchini Iraq.

Kiongozi wa juu wa Iran Ayatollah Ali Khamenei aliapa kulipiza kisasi na kutangaza siku tatu za maombolezi.

Hata hivyo Trump aliionya Iran na kusema Marekani itayalenga maeneo 52 ambayo ni muhimu sana kwa Iran, na kwamba itawashambulia haraka na kwa namna ambayo hawajawahi kushuhudia.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.