Pata taarifa kuu
LEBANON-USALAMA-SIASA

Mazungumzo kuhusu uundwaji wa serikali mpya kuanza Lebanon

Mashauriano ya wabunge yaliyoshirishwa mara kadhaa nchini Lebanon kwa minajili ya kuunda serikali mpya yamepangwa kuanza Alhamisi, Desemba 19.

Waziri Mkuu aliyejiuzulu Saad Hariri pamoja na Rais wa Lebanon Michel Aoun, Novemba 22, 2019.
Waziri Mkuu aliyejiuzulu Saad Hariri pamoja na Rais wa Lebanon Michel Aoun, Novemba 22, 2019. REUTERS/Mohamed Azakir
Matangazo ya kibiashara

Waziri Mkuu Saad Hariri aliyejiuzulu, amebaini kwamba, hatowania kwenye wadhifa huo. Katika siku za hivi karibuni, maaandamano yalikumbwa na vurugu, na kusababisha hasara.

Katika mji mkuu wa Lebanon, Beirut, hatua za kiusalama zimeanza kutumika tangu Jumatano, Desemba 18, ambapo yanaendelea maandamanao yanayoendelea kuikumba nchi hiyo kwa miezi miwili.

Katika usiku wa hivi karibuni, vurugu ziliibuka katika mji mkuu wa Lebanon. Watu kadhaa walijeruhiwa katika makabiliano kati ya waandamanaji na vikosi vya usalama.

Kumekuwa na makabiliano kati ya waandamanaji na vikosi vya usalama. Mapigano mengine yaliripotiwa kati ya waandamanaji na waandamanaji wengine wanaotambuliwa kama wafuasi wa kundi la wanamgambo wa Kishia wa Hezbollah. Katka moji mingine kumetokea makabiliano kati ya wanamgambo hao wafuasi wa Hezbollah na vikosi vya usalama.

Jumatano wiki hii, waziri mkuu aliyejiuzulu, Saad Hariri, amesema Jumatano kwamba hatowania kwenye wadhifa huo. Wengi walipendelea aendelee kuhudumu kama waziri mkuu, lakini amekataa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.