Pata taarifa kuu
SYRIA-USALAMA

Syria: Mapigano makali katika mkoa wa Idleb yatatiza utekelezwaji wa usitishwaji mapigano

Mkataba wa kusitisha mapigano katika mkoa wa Idleb, Kaskazini magharibi mwa Syria, umedhoofishwa na mapigano ya siku mbili za kati ya vikosi vya serikali na mkundi ya wanajihadi na waasi.

Ndege za kivita zilizindua mashambulizi kadhaa kwenye maeneo yaliyo karibu au mbali na mapigano.
Ndege za kivita zilizindua mashambulizi kadhaa kwenye maeneo yaliyo karibu au mbali na mapigano. Omar HAJ KADOUR / AFP
Matangazo ya kibiashara

Siku mbili za mapigano kati ya vikosi vya serikali na makundi yenye silaha katika ngome ya mwisho ya waasi nchini Syria, yamesababisha vifo vya takriban watu 70 kutoka pande zote mbili, mashahidi wamebaini.

Kwa mujibu wa shirika la Haki za Binadamu nchini Syria (OSHR), mapigano hayo ya siku mbili zilizopita katika mkoa wa Idleb yamesababisha vifo vya watu zaidi ya 80, ikiwa ni pamoja na wapiganaji zaidi ya 70.

Mkuu wa shirika hilo la kufuatilia haki za binadamu la Syria, amesema kuwa mapigano katika mkoa wa Kaskazini Magharibi wa Idlib ndio mabaya zaidi nchini humo tangu makubaliono ya kusitisha mashambulizi yaliosimamiwa na Urusi kuanza kutekelezwa mwishoni mwa mwezi Agosti.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.