Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 18/01 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 18/01 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 17/01 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Mashariki ya Kati

Trump atangaza kuanza tena kwa mazungumzo na Taliban

media Akizuru kambi ya kikosi cha jeshi la wanaanga la Marekani huko Bagram, Rais wa Marekani Donald Trump amekutana naRais wa Afghanistan Ashraf Ghani na kula chakula cha jioni na askari wa Marekani. REUTERS/Tom Brenner

Rais wa Marekani, Donald Trump ametangaza wakati wa ziara yake ya kushtukiza usiku katika kambi ya kikosi cha jeshi la Marekani nchini Afghanistan kwamba mazungumzo na Taliban, yaliyositishwa mwezi Septemba, yameanza tena.

Ziara hii ya Bw Trump, ambayo ni ya kwanza nchini humo, ilikuwa ya kushtukiza kwa sababu za usalama.

"Wataliban wanataka mkataba, na tunakutana nao, tumewaambia kuwa tunataka kusitishwa kwa mapigano, awali hawakutaka kusitisha mapigano, na sasa wanataka kusitisha mapigano," amesema Donald Trump baada ya kukutana na mwenzake wa Afghanistan Ashraf Ghani, katika kambi ya kikosi cha jeshi la wanaanga la Marekani ya Bagram, kilomita 80 kaskazini mwa Kabul.

"Nadhani kwa uhakika hii ni njia nzuri," amebaini rais wa Marekani.

"Tutasalia hivi mpaka mpale tutakuwa na mkataba au mpaka pale tutapata ushindi kamili, na wanataka kweli kufikia mkataba," Donald Trump ameongeza.

Rais wa Marekani amebaini kwamba anataka kupunguza idadi ya askari wa Marekani kutoka kati ya 13,000 na 14,000 leo hadi 8,600.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana