Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 25/01 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 25/01 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 25/01 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Mashariki ya Kati

Waziri Mkuu wa Israeli Benyamin Netanyahu ashtakiwa

media Waziri Mkuu wa Israeli Benyamin Netanyahu, Mei 30, 2019. REUTERS/Ronen Zvulun

Mwanasheria mkuu nchini Israeli ametangaza kwamba Waziri Mkuu wa nchi hiyo Benyamin Netanyahu amefunguliwa mashitaka kwa makosa ya rushwa, ufisadi na kuvunjwa uaminifu katika kesi tatu tofauti.

Benyamin Netanyahu ni kiongozi wa kwanza wa serikali katika historia ya nchi hiyo kushtakiwa wakati bado yuko madarakani.

Benyamin Netanyahu hataishia hapo. Kustakiwa kwake ni "jaribio la mapinduzi", waziri mkuu wa Israel amesema.

Usiku wa leo, tunashuhudia jaribio la mapinduzi dhidi ya Waziri Mkuu kwa tuhuma za uwongo na kutumia mfumo uliopitwa na wakati wenye upendeleo. Napenda kuwambia kwamba siku hii ni siku ngumu sana. Na ninajua kuwa ni huzuni mkubwa kwa Waisrael wengi ambao wananiunga mkono na ambao wananipenda. Sitakubali ushindi wa uwongo. Nitaendelea kuongoza nchi hii kama inavyosema sheria. Na tunapaswa kufanya jambo moja: Tunapaswa kufanya kuchunguza wanaoendesha uchunguzi, Benyamin Netanyahu amesema

Mashtaka haya ni ya kwanza kwa waziri mkuu wa Israeli aliye madarakani. Benyamin Netanyahu anashtakiwa katika kesi tatu tofauti. Kesi kubwa zaidi, ni ile inayohusu kampuni ya mawasiliano ya Bezeq.

Waziri mkuu huyo anadaiwa kupokea zawadi kutoka kwa mfanyabiashara tajiri na kukubali upendeleo wa kupata nafasi ya kuchapishiwa taarifa zake.

Madai mengine anayoshtakiwa nayo bwana Nyetanyahu ni kupokea zawadi ya kiasi cha dola za Marekani 264,100 kutoka kwa msanii wa Hollwood mwenye asili ya Israel Arnon Milchan na pamoja na bilionea wa Australia James Packer.

Zawadi kutoka kwa Bwana Milchan, ni madai ya kutaka amsaidie kupata visa ya Marekani na pia katika masuala ya kodi.

Hata hivyo Milchan na Packer wameyakana mashtaka yao.

Mwanasheria mkuu wa serikali Avichai Mandelblit amesema atazingatia mashtaka ya ufisadi na kuvunja uaminifu, pamoja na rushwa.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana