Pata taarifa kuu
ISRAELI-PALESTINA-USALAMA

Israeli yafanya mashambulizi mapya dhidi ya ngome ya wanajihadi Gaza

Jeshi la Israeli linasema limetekeleza mashambulizi mapya katika ngome za wanajihadi katika eneo la Gaza, baada ya roketi kadhaa kurushwa katika ardhi ya Israel licha ya kuwepo kwa makubaliano ya kuwepo kwa utulivu.

Wiki hii makabiliano kati ya jeshi la Israel na wapiganaji wa Kipalestina yalishuhudiwa katika eneo la Gaza, baada ya Israel kumuua, Kamanda wa kundi la Kijihadi.
Wiki hii makabiliano kati ya jeshi la Israel na wapiganaji wa Kipalestina yalishuhudiwa katika eneo la Gaza, baada ya Israel kumuua, Kamanda wa kundi la Kijihadi. AFP/BASHAR TALEB
Matangazo ya kibiashara

Kupitia taarifa yake kwa wanahabari, kupitia mtandao wa kijamii wa WhatsApp, jeshi la Israeli linasema linashambulia Gaza kuanzia asubuhi ya leo Ijumaa.

Wiki hii makabiliano kati ya jeshi la Israeli na wapiganaji wa Kipalestina yalishuhudiwa katika eneo la Gaza, baada ya Israeli kumuua, Kamanda wa kundi la Kijihadi.

Hata hivyo, Misri iliiangilia kati mapigano hayo na kusaidia kuleta utulivu kati ya pande hizo mbili, hali ambayo inatarajiwa kubadilika baada ya Israeli kuanzisha mashambulizi mapya.

Mapigano ya wiki hii kwa mujibu wa Madaktari wa Kipalestina, yamesababisha vifo vya watu 34, wote raia wa Palestina wakiwemo watoto wanane na wanawake watatu.

Israeli nayo inasema wanajeshi wake zaidi ya 60 wamejeruhiwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.