Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 21/02 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 21/02 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 18/02 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Mashariki ya Kati

Kundi la Islamic State lamtangaza kiongozi wake mpya

media Picha iliyotolewa na kundi la Islamic State Aprili 29, 2019 ikimuonyesha Abu Bakr al-Baghdadi. Islamic State Group/Al Furqan Media Network/Reuters TV

Kundi la Islamic State limethibitisha kifo cha kiongozi wake Abu Bakr al-Baghdadi, aliyeuawa katika operesheni ya jeshi la Marekani nchini Syria, na kumtangaza mrithi wake kwa kutishia Marekani kulipiza kisasi.

Uthibitisho wa kifo cha Abu Bakr al-Baghdadi ulitolewa katika ujumbe wa sauti uliowekwa kwenye programu ya Telegraph. "Enyi Waislamu, Enyi Wanajihadi, askari wa IS (...), tunahuzunishwa na kifo cha mkuu wa waumini Abu Bakr al-Baghdadi", ametangaza Abu Hamza Al-Qurachi, aliyetambulishwa kama msemaji mpya wa kundi lenye msimamo mkali la IS.

Uthibitisho huu unakuja siku tano baada ya Donald Trump kutangaza kifo cha Abu Bakr al-Baghdadi katika operesheni ya jeshi la Marekani nchini Syria. Katika sauti yake ya dakika saba iliyorekodiwa, msemaji mpya wa kundi hili la wanajihadi ametoa wito wa kulipiza kisasi kwa kifo hicho, haswa akitishia Marekani kulipiza kisasi na kumuita rais wa nchi hiyo "mzee mpumbavu."

"Marekani usifurahi na kujigamba, anakuja mtu ambaye atakufanya usahau mambo uliomfanyia," Abu Bakr al-Baghdadi na "kukukatikiza kiu cha mabaya unayofanyia ulimwengu(...) ambapo utakuja kuonekana mtu mwenye unyonge na masikitiko makubwa" , ameongeza Abu Hamza Al-Qurachi.

Kundi la Islamic State limebaini katika ujumbe huo wa sauti kwamba mkutano wa mashauriano wa kundi hilo, Majlis al-Shura, umeapa kumtii na kumuunga mkono Abu Ibrahim al-Hashemi al-Qurachi, "kiongozi mkuu wa waumini" na "khalifa mpya wa Waislamu". Jina hili halikuwa limetajwa miongoni mwa watu waliopewa nafasi kubwa kumrithi Baghdadi.

"Hatujui mengi kuhusu yeye, isipokuwa tu kwamba yeye ndiye jaji mkuu wa IS na ndiye kiongozi wa Mamlaka ya

Sharia," Hicham al-Hachemi, mtaalam wa masuala ya kijihadi ameliambia shirika la Habari la AFP.

Abu Bakr al-Baghdadi, kiongozi wa kundi la Kijihad la Islamic State (IS) na mtu ambaye alikuwa akisakwa sana duniani , alijiua kufuatia uvamizi wa Marekani uliotekelezwa na kikosi maalum cha wanajeshi kaskazini magharibi mwa Syria.

Kiongozi huyo aliyejiita 'Kalifa Ibrahim' alikuwa amewekewa dola milioni 25 kwa mtu yeyote ambaye angefichua maficho yake na alikuwa akisakwa na Marekani na washirika wake tangu kuanzishwa kwa kundi la IS miaka mitano iliopita.

Baghdadi aliapishwa kuwa kiongozi wa kundi hilo mwaka 2014 wakati ambao wanamgambo wa IS walipoweza kuishinda Iraq na Syria na kuanzisha utawala wao mpya wao.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana