Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 21/11 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 21/11 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 20/11 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Mashariki ya Kati

Syria: Putin akutana na Erdogan ambaye anatishia kuanzisha tena mashambulizi

media Rais wa Uturuki Erdogan na Rais wa Urusi Putin wamekutana Sochi Jumanne, Oktoba 22 kabla tu ya kumalizika kwa muda wa kusitisha mapigano katika mashambulizi ya Uturuki nchini Syria. Reuters/Mustafa Kamaci/Turkish Presidential Press Office/

Rais wa Urusi Jumanne wiki hii amempokea mwenzake wa Uturuki na wamejadili kuhusu mazungumzo yanayohusu mapigano kaskazini mashariki mwa Syria.

Wakati huo huo serikali ya Ankara imetishia kuanza tena mashambulizi dhidi ya wapiganaji wa Kikurdi kabla tu ya kumalizika kwa muda wa kusitisha mapigano.

"Hali katika kanda hii ni mbaya sana," Vladimir Putin amesema mwanzoni mwa mkutano wake na Recep Tayyip Erdogan, akimtaka "kupata suluhisho hata kwa maswala magumu zaidi".

Alipowasili Sochi, Erdogan amesema ana matumaini kuwa mazungumzo hayo yatakuwa na "nafasi thabiti kwa kudumisha amani" kwani Ankara inataka wapiganaji wa Kikurdi kuondoka kaskazini mashariki mwa Syria, pamoja na katika maeneo yaliyo chini ya udhibiti wa serikali ya Syria inayoungwa mkono na Moscow.

Hivi karibuni, Waziri wa mambo ya nje wa Uturuki, Mevlüt Çavuşoğlu, alifahamisha kwamba sio kusitisha mapigano bali ni “kuwapa muda wapiganaji wa PYD tawi la kundi la kigaidi la PKK kuondoka katika mipaka ya Uturuki na Irak na Syria.

Waziri wa mambo ya nje wa Uturuki alisema kuwa makubaliano na tume hiyo kutoka Marekani kuhusu PYD ni kuwapokonya silaha nzito na kuondoa kambi zao wanazotumia kushambulia Uturuki.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana