Pata taarifa kuu
SYRIA-USALAMA

Syria: Vikosi vya Marekani havitapiga kambi tena karibu na mpaka wa Uturuki

Marekani imetangaza Jumapili usiku kwamba Uturuki itaongoza "hivi karibuni" operesheni ya jeshi kuingia kaskazini mwa Syria na kwamba vikosi vyake vilioko nchini vitaondoka karibu na eneo ambako operesheni hiyo itaendeshwa.

Magari ya jeshi la Uturuki na Marekani yakipiga doria karibu na mji wa Tal Abyad, nchini Syria, karibu na mpaka wa Uturuki, Oktoba 4, 2019.
Magari ya jeshi la Uturuki na Marekani yakipiga doria karibu na mji wa Tal Abyad, nchini Syria, karibu na mpaka wa Uturuki, Oktoba 4, 2019. © AFP
Matangazo ya kibiashara

Ikulu ya White House imetoa tangazo hilo la kushangaza, kufuatia mazingira magumu ya kutathmini, kwa kuripoti mazungumzo ya simu kati ya Rais wa Marekani Donald na mwenzake wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan.

"Uturuki hivi karibuni itafanya operesheni yake iliyopangwa kwa muda mrefu kaskazini mwa Syria," msemaji wa White House Stephanie Grisham amesema katika taarifa.

"Vikosi vya Marekani havitaunga mkono au kuhusika katika operesheni hiyo na vikosi vya Marekani, ambavyo vilishinda kundi la Islamic State kwa kuondoa wapiganaji wa kundi hilo katika maeneo yaliyokuwa chini ya udhibiti wake, havitakuwa tena karibu na maeneo amako operesheni ya kijeshi ya Uturuki itaendeshwa," amebainisha msemaji wa ikulu ya White House.

Ikulu ya White House haikuelezea chochote juu ya operesheni hii ya Uturuki, ambayo wigo wake bado haueleweki, na athari zake kwa wapiganaji wa Kikurdi, ambao ni washirika wa Washington, ambao waliwezesha mafanikio ya kijeshi dhidi ya kundi la Islamic State (IS).

Kwenye ukurasa wake wa Twitter, muungano wa wapiganaji wa Kiarabu na Kikurdi, FDS, wamepinga uamuzi wa Marekani na hatua ya Uturuki kuingia kijeshi nchini Syria.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.