Pata taarifa kuu
IRAQ-USALAMA

Maandamano Iraq: waandamanaji wanane wauawa wakati wa makabiliano Baghdad

Waandamanaji wanane wameuawa katika makabiliano mapya jana Jumapili na vikosi vya usalama jijini Baghdad, siku ya sita ya maandamano yaliyogubikwa na vurugu ambao zimesababisha watu zaidi ya100 kupoteza maisha na maelfu kujeruhiwa nchini Iraq.

Vijana wakiandamana katika mitaa ya Baghdad, Oktoba 4, 2019.
Vijana wakiandamana katika mitaa ya Baghdad, Oktoba 4, 2019. REUTERS/Alaa al-Marjani
Matangazo ya kibiashara

Makabiliano haya yalitokea licha ya serikali kutangaza hatua kadhaa za kijamii kujibu madai ya waandamanaji wanaotaka serikali kujiuzulu.

Waandamanaji wanashtumu serikali kujihusisha na ufisadi, na kufanya mageuzi ya kiuchumi bila kuzingatia maslahi ya wananchi.

Kwa mujibu wa vyanzo vya usalama, makabiliano kati ya waandamanaji na polisi yalizuka katika mji wa Sadr, ngome ya kiongozi wa Kishia Moqtada Sadr ambaye Ijumaa aliitaka serikali kujiuzulu. Waandamanaji wanane waliuawa, polisi na vyanzo vya hospitali vimesema.

Wakati wa makabiliano, milio ya risasi ilisikika, huku waandamanaji wakichoma matairi na kurusha vifaa vya moto kwa vikosi vya usalama, mashahidi wamesema.

Kulingana na ripoti ya hivi karibuni iliyotolewa na msemaji wa Wizara ya Mambo ya Ndani, watu 104, ikiwa ni pamoja na askari wanane, wameuawa na zaidi ya 6,000 kujeruhiwa tangu kuibuka kwa maandamano ya Jumanne. Wengi wa waliouawa ni waandamanaji, ambao wengi wao waliuawa kwa kupigwa risasi, kulingana na vyanzo vya hospitali.

Haijulikani wazi ikiwa watu hao wanane waliouawa Jumapili usiku wamejumuishwa kwenye iadai iliyotoleawa na Wizara ya Mambo ya Ndani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.