Pata taarifa kuu
YEMEN-USALAMA

Mashambulizi ya muungano wa nchi za Kiarabu yaua watu zaidi ya 100 Yemen

Chama cha msalaba mwekundu na mwezi mwekundu (ICRC) nchini Yemen kimebaini kwamba zaidi ya watu 100 wameuawa katika mashambulizi yaliyoendeshwa na muungano wa nchi za Kirabu nchini humo.

Madaktari wa Chama cha msalaba mwekundu na mwezi mwekundu (ICRC)kwenye eneo la mashambulizi, Dhamar, Yemen, Septemba1, 2019.
Madaktari wa Chama cha msalaba mwekundu na mwezi mwekundu (ICRC)kwenye eneo la mashambulizi, Dhamar, Yemen, Septemba1, 2019. REUTERS/Mohamed al-Sayaghi TPX IMAGES OF THE DAY
Matangazo ya kibiashara

Muungano unaoongozwa na Saudi Arabia uliendesha mashambulizi dhidi ya kituo wanakozuiliwa wafungwa kinachoshikiliwa na waasi wa Houthi, kusini mwa mji mkuu Sana'a, kwa mujibu wa mashahidi.

Jumapili asubuhi, muungano wa nchi za Kiarabu, kwa upande wake, ulitangaza kwamba uliendesha mashambulizi ya anga dhidi ya "ngome ya kijeshi ambako kunahifadhiwa ndege ziszo kuwa na rubani na makombora" katika jiji la Dhamar, magharibi mwa nchi, kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na televisheni ya Saudi Arabia, Al-Ekhbariya.

"Tunakadiria kuwa zaidi ya watu 100 wameuawa" katika mashambulizi haya, amesema Franz Rauchenstein, mkuu wa ICRC nchini Yemen, ambaye alizuru eneo la tukio.

Watu wasiopungua 40 waliojeruhiwa wamelazwa katika hospitali kadhaa jijini Dhamar, Franz Rauchenstein ameongeza. Awali alibaini kwamba jengo lililolengwa lilikuwa "mahali wanakozuiliwa wafungwa" ambapo ICRC tayari imetembelea mara kadhaa. Kwenye ujumbe wa Twitter, ICRC nchini Yemen imebaini kwamba ilibeba katika eneo la mashambulizi mifuko 200 ya kuhifadhi miili ya watu waliouawa katika mashambulizi hayo.

Kwa upande wake, kundi la waasi la Houthi, kwenye televisheni yake ya Al-Masirah, limedai kwamba "watu wengi waliuawa na wengine kujeruhiwa" katika mashambulizi saba, likisema kwamba jengo linalotumiwa kama gereza lililengwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.