Pata taarifa kuu
IRAN-MAREKANI-UFARANSA-UN

Iran kuanza kurutubisha madini ya Uranium

Iran inatarajiwa kuongeza kiwango cha kurutubisha uranium kuanzia tarehe 27 mwezi Juni, kwa mujibu wa makubaliano ya mkataba  uliokubaliwa kati yake na mataifa ya Magharibi.

Rais wa Iran Hassan Rouhani
Rais wa Iran Hassan Rouhani REUTERS/Abdullah Dhiaa Al-Deen
Matangazo ya kibiashara

Afisa wa serikali ya Iran, Behrouz Kamalvandi anayehusika na masuala ya atomic, amesema kuwa ndani ya siku 10 zijazo, Tehran itaanza kuongeza kiwango hicho.

Kifungu cha mkataba huo kinaeleza kuwa, mkataba huo unaweza kupitiwa upya iwapo wanachama walioutia saini watakuwa wametekeleza majukumu yao.

Mwezi May, rais Hassan Rouhani alitangaza kuwa Iran itaacha kuheshimu vikwazo vya kutoendelea na urutubishaji wa uranium kwa mujibu wa mkataba huo.

Tangu kuingia madarakani mwaka 2016, serikali ya Marekani chini ya uongozi wa rais Donald Trump, imekataa kuendelea kuheshimu mkataba huo na badala ya kujiondoa na kuyaacha mataifa mengine kama Uingereza, China, Ufaransa, Ujerumani na Urusi.

Marekani imeendelea kuiwekea vikwazo vya kiuchumi Iran, baada ya kujiondoa kwenye mkataba huo ambao ulikubaliwa kuwa, ungedumu kwa muda wa miaka 10.

Mwaka 2015, Iran na Mataifa yenye nguvu duniani, yaliingia kwenye mkataba ulioitaka Iran kuachana na mpango wake wa kurutubisha uranium ili kupunguza uwezo wake kutengeza silaha nyuklia ambazo zitakuwa tishio kwa dunia.

Hata hivyo, Iran imekuwa ikisema mpango wake ni wa amani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.