Pata taarifa kuu
SAUDIA-YEMEN-USALAMA

Mali muhimu za Saudi Arabia zashambuliwa Yemen

Waasi wa Houthi nchini Yemen wamezindua mashambulizi kwa kutumia ndege zisizo na rubani dhidi ya mali muhimu ya Saudi Arabia, kituo cha televisheni kinachomilikiwa na kundi Mashia wanaoungwa mkono na Iran kimetangaza Jumanne wiki hii.

Meli mbili za Saudi Arabia zilizokuwa zikisheheni mafuta zimeshambuliwa na watu wasiojulikana. Tayari kundi la waasi wa Houthi wamedai kuwa wao ndio walihuska na shambulio hilo.
Meli mbili za Saudi Arabia zilizokuwa zikisheheni mafuta zimeshambuliwa na watu wasiojulikana. Tayari kundi la waasi wa Houthi wamedai kuwa wao ndio walihuska na shambulio hilo. Β© Reuters
Matangazo ya kibiashara

Kituo cha televisheni cha Massirah, ambacho kimenukuu askari wa Houthi, hakikusema tarehe ya shambulio wala vitu vilivyolengwa.

"Hii operesheni muhimu ya kijeshi ni jibu kwa uchokozi unaoendelea na dhulma kwa raia wetu na tuko tayari kuendeleza mashambulizi makubwa ya angani," amesema askari huyo aliyenukuliwa na Al Massirah kwenye Twitter.

Saudi Arabia, ambayo haijathibitisha taarifa hii, siku ya Jumatatu ilitangaza kwamba meli zake mbili zilizoshehi mafuta ni miongoni mwa meli nne zilizolengwa na mashambulizi kwenye Pwani ya Falme za Kiarabu Jumapili Mei 12, 2019.

Haijulikani kama waasi wa Houthi, ambao wako katika vita nchini Yemen dhidi ya muungano wa nchi zenye dhehebu la Sunni, unaoongozwa na Saudi Arabia na Falme za Kiarabu, wametaka kudai kuhusika na shambulio la Jumapili, lililotokea karibu na mji wa Fujairah katika Falme za Kiarabu.

Mamlaka za Falme ya Kiarabu hazikubaini aina ya shambulio hilo wala aliyehusika na shambulio.

Waasi wa Houthi ambao mara kwa mara wamekuwa wakifanya mashambulizi kwa kutumia ndege zisizo na rubani dhidi ya Saudi Arabia, wamedai kufanya mashambulizi kama hayo dhidi ya Falme za Kiarabu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.