Uhuru wa Israeli kuhusu Milima ya Golan: Saudi Arabia yalaani msimamo wa Marekani
Saudi Arabia imeshutumu uamuzi wa Donald Trump kutambua uhuru wa Israeli kuhusu Milima ya Golan kama ukiukwaji wa mkataba wa kimataifa na azimio la kimataifa.
Imechapishwa:
Saudi Arabia imefutilia mbali uamuzi huo na kulani tangazo la utawala wa Marekani kutambua uhuru wa Israeli kuhusu Milima ya Golan upande wa Syria inayokaliwa na Wayahudi," shirika la Habari la SPA limeripoti.
Golan itabaki kiuwa ardhi ya Syria "inayokaliwa na Wayahudi" na kutambua eneo hilo kama sehemu ya ardhi ya Israeli ni "ukiukwaji mkubwa wa Mkataba wa Umoja wa Mataifa na azimio la kimataifa," Saudi Arabia imeongeza.
"Kutakuwa na athari mbaya juu ya mchakato wa amani katika Mashariki ya Kati, pamoja na usalama na utulivu katika ukanda huo," taarifa ya Saudi Arabia imebaini.
Israeli ilitawala sehemu kubwa ya kubwa ya eneo la Golan nchini Syria (kilomita mraba 1,200) wakati wa Vita ya Siku sita mnamo mwaka 1967, kabla ya kulifanya kuwa moja ya sehemu zake za ardhi mnamo mwaka 1981. Eneo hilo halijatambuliwa na jumuiya ya kimataifa kama sehemu ya Israeli.