Mauaji ya Khashoggi: Umoja wa Mataifa washtumu utawala wa kifalme wa Saudia
Katika taarifa yake, Agnes Callamard, kiongozi wa maafisa wa uchunguzi wa Umoja wa Mataifa ameshtumu utawala wa Kifalme wa Saudi Arabia kuhusika na kifo cha mwandishi wa habari Jamal Khashoggi.
Imechapishwa:
Jamal Khashoggi aliuawa Oktoba 2, 2018 katika ubalozi mdogo wa Saudi Arabia, jijini Istanbul, nchini Uturuki.
Maafisa wa uchunguzi wa Umoja wa Mataifa wamebaini kwamba mauaji ya Jamal Khashoggi "yalipangwa" na utawala wa Saudi Arabia na ni "ukiukwaji mkubwa wa haki ya msingi kuliko nyingine, haki ya kuishi".
Pia Agnes Callamard amelaani matumizi ya "kinga" ya kidiplomasia kufanya mauaji ya "kikatili".
"Ushahidi uliokusanywa wakati wa ziara yangu nchini Uturuki unaonyesha ... kwamba Bw Khashoggi, mauaji yake ya kikatili yalipangwana wawakilishi wa utawala wa Kifalme wa saudi Arabia," amesema Agnes Callamard, akinukuliwa katika taarifa hiyo.
Zaidi ya miezi minne baada ya kifo chake, mwili wa mwandishi wa habari wa Washington Post, bado haujapatikana. Mauaji yake yaliitumbukiza Saudi Arabia katika mogogoro mkubwa wa kidiplomasia na kuchafua jina la mwanamfalme Mohammed bin Salman ambaye anashtumiwa na maafisa wa Marekani na Uturuki kutoa agizo kwa mauaji hayo.