Pata taarifa kuu
AFGHANISTAN-TALIBAN-USALAMA

Afghanistan yatoa wito kwa Taliban kushiriki mazungumzo ya moja kwa moja

Mazungumzo kati ya Taliban na Marekani wiki iliyopita mjini Doha yameleta matumaini ya mkataba wa amani ambao unatarajia kumaliza miaka 17 ya vita vya wenyewe kwa wenyewe.

Rais wa Afghanistan Ashraf Ghani akikutana na Mwakilishi Maalum wa Marekani Zalmay Khalilzad katika ikulu ya Kabul, Januari 28, 2019.
Rais wa Afghanistan Ashraf Ghani akikutana na Mwakilishi Maalum wa Marekani Zalmay Khalilzad katika ikulu ya Kabul, Januari 28, 2019. Handout / Afghan Presidential Palace / AFP
Matangazo ya kibiashara

Wakati pande zote mbili zimesema kuwa zimepata mafanikio makubwa, hatua muhimu zaidi ya miaka tisa iliyopita, bado kuna tofauti kati ya pande hizo mbili.

Hata hivyo Pentagon inasem akuna ulazima kuepo na mazungumzo kati ya serikali na Taliban katika hali ya kumaliza kabisa migogoro nchini Afghanistan.

Baada ya siku sita za mazungumzo, Taliban wameahidi kuchukua hatua za kuzuia Afghanistan kuwa kama eneo la ugaidi wa kimataifa. Kutokana na msimamao huo wa Taliban, Marekani imeahidi kuondoa askari wake nchini Afghanistan. Kwa sasa, haijulikani jinsi ratiba ya kuondoka kwa askari wa Maekani nchini Afghanistan na taratibu za kusitisha mapigano.

Bado kuna kikwazo kikubwa sasa: kuishawishi Taliban kuzungumza moja kwa moja na serikali ya Afghanistan. jambo ambalo Taliban imeendelea kupinga.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.