Matamshi ya Pompeo ameyatoa wakati huu akianza ziara katika mataifa ya kiarabu kuyapa hakikisho kuwa nchi yake itaendelea na vita dhidi ya kundi hilo licha ya kutangaza mpango wa kuanza kuwaondoa wanajeshi wake nchini Syria.
Ziara ya Pompeo inakuja wakati huu maofisa kadhaa wa juu katika wizara ya ulinzi ya Marekani wakitangaza kujiuzulu nafasi zao, majuma kadhaa baada ya rais Donald Trump kutangaza kuwaondoa wanajeshi wake nchini Syria akisema kundi la Islamic State limedhibitiwa.
Pompeo anatembelea nchi za kiarabu ikiwa ni siku chache tu tangu mshauri wa masuala ya usalama wa taifa wa Marekani John Bolton, afanye ziara nchini Israel na Uturuki kuwahakikishia nchi washirika kuwa vita dhidi ya Islamic State itaendelea.