Pata taarifa kuu
SYRIA-URUSI-ISRAEL-USALAMA

Moscow yashutumu Israeli kufanya mashambulizi Syria

Urusi imeishtumu Israel kwa kutishia uhuru wa Syria, na kuhatarisha kuanguka kwa ndege mbili za abiria, baada ya kushambulia ghala la kuhifadhi silaha la nchi hiyo jijini Damascus.

Waziri Mkuu wa Israel Netanyahu akiongea mbele kikosi cha wanaanga cha Israeli katika kambi ya Hatzerim tarehe 26 Desemba 2018.
Waziri Mkuu wa Israel Netanyahu akiongea mbele kikosi cha wanaanga cha Israeli katika kambi ya Hatzerim tarehe 26 Desemba 2018. REUTERS/Amir Cohen/File Photo
Matangazo ya kibiashara

Moscow inasema, kitendo cha Israel ni uchokozi kwa mshirika wake Syria, lakini Israel imejitetea kwa kusema kuwa ilifanya mashambulizi hayo kwa kujilinda.

Urusi imethibitisha kwamba serikali ya Kiyahudi ndio imefanya mashambulizi ya makombora katika nchi ya Syria siku ya Jumanne, Desemba 25.

Urusi kupitia wizara yake ya Ulinzi imetaja kitendo hicho kama "Ukiukwaji mkubwa" wa uhuru wa Syria.

Kwa upande wa Urusi, "mashambulizi hayo" ni kitendo cha uchokozi kilichofanywa na jeshi la Israeli Jumanne usiku, na kulenga ardhi ya Syria. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa Jumatano na wizara ya Ulinzi ya Urusi, "ndege sita za kivita za jeshi la Israeli ziliendesha mashambulizi ya makombora katika kitongoji cha Damascus usiku wa kuamkia tarehe 25 Desemba".

Ni "ukiukwaji mkubwa wa uhuru wa Syria," imesema Urusi, huku ikishutumu Israeli kuhatarisha usalama wa ndege mbili uza abiria zilizokuwa zinaelekea Beirut na Damascus.

Israeli imefanya mashambulizi mengi nchini Syria tangu kuzua vita mnamo mwaka 2011, ikilenga vikosi vya Rais Bashar al-Assad lakini pia washirika wake, ikiwa ni pamoja na majeshi ya Irani au ngome zawapiganaji wa Hezbollah kutoka Lebanoni.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.