Pata taarifa kuu
ISRAEL-AUSTRALIA-PALESTINA-JERUSALEM

Australia yatambua Jerusalem Magharibi kama makao makuu ya Israel

Australia imetangaza kuwa inatambua Jerusalem Magharibi, kama mji mkuu wa Israel.

Waziri Mkuu wa Australia Scott Morrison
Waziri Mkuu wa Australia Scott Morrison REUTERS/David Gray
Matangazo ya kibiashara

Tangazo hili limetolewa na Waziri Mkuu Scott Morrison ambaye hata hivyo amesema kuwa, nchi yake haitahamisha Ubalozi wake Jerusalem, had pale mkataba wa amani utakapopatikana kati ya Waisraeli na Wapalestina.

Aidha, Scott amesema nchi inadhamiria kutambua Mashariki mwa Jerusalem kuwa makao makuu ya Wapalestina.

Marekani ilikuwa ya kwanza kutambua Jerusalem kuwa mji Mkuu wa Israel na mwezi Mei, ilihamisha ubalozi wake kutoka Tel Aviv licha ya kushtumiwa kimataifa.

Kimataifa, Jerusalem haijawahi kutambuliwa kuwa mji mkuu wa Israel kwa mujibu wa makubaliano ya amani ya mwaka 1993, kati ya Israel na Palestina.

Israel imeendelea kusema Jerusalem ndio mji wake mkuu na umeendelea kujenga makaazi Mashariki mwa mji huo, hatua ambayo imeendelea kuikera Palestina.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.