Pata taarifa kuu
YEMEN-UN-USALAMA-MAZUNGUMZO

Makubaliano ya kusitisha mapigano Hodoidah yafikiwa

Pande zinazohasimiana nchini Yemen zimekubaliana kusitisha mapigano kwenye mji wa bandari wa Hodoidah, makubaliano ambayo Umoja wa Mataifa umesema yatasaidia kumaliza hali mbaya ya kibinadamu katika taifa hilo.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres katika mkutano na waandishi wa habari unaohitimisha mazungumzo ya amani ya Yemen huko Rimbo, karibu na Stockholm, tarehe 13 Desemba 2018.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres katika mkutano na waandishi wa habari unaohitimisha mazungumzo ya amani ya Yemen huko Rimbo, karibu na Stockholm, tarehe 13 Desemba 2018. TT News Agency/Pontus Lundahl via REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres, amesema waasi wa Huthi wamekubali kuondoka kwenye mji huo na kukubali pia kuachia maeneo matatu ya bandari ambayo yalikuwa kiini cha ustawi wa jamii ya Yemen.

Guterres ameongeza kuwa makubaliano haya ni hatua muhimu katika kuhakikisha amani ya kudumu inapatikana kwenye taifa hilo.

Katika makubaliano haya maeneo yote ya bandari yatakuwa chini ya askari wa eneo hilo ambao watakusanya mapato na kuyatuma katika benki kuu ya nchi hiyo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.