Pata taarifa kuu
UFARANSA-SAUDI ARABIA-USHIRIKIANO

Rais wa Ufaransa kukutana na Mwanamfalme Salman

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron amesema kuwa atakutana kwa mazungumzo ya faragha na Mwanamfalme Salman kando na mkutano wa mataifa yenye viwanda na yale yanayoinukia kiviwanda G20, nchini Argentina.

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron.
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron. REUTERS/Agustin Marcarian
Matangazo ya kibiashara

Macron amewaambia waandishi wa Habari kuwa lengo lake ni kuhakikisha anapata maelezo kamili kuhusu mauaji ya mwanadishi wa habari Jamal Kashoggi aliyeuawa katika mazingira yenye kutatanisha katika ubalozi mdogo wa Saudi Arabia nchini Uturuki.

“ Kila mara Nimekuwa muwazi sana kuhusu Saudi Arabia na nitakuwa na nafasi ya kuzungumzia hili pale ambapo nitakutana na Mwanamfalme Salman, mbali na mkutano wa G20 : Naamini sitakosa nafasi hii. Kwanza kuna suala la mauaji ya Khashoggi ambalo ni suala ngumu; na nitahitaji ukweli wote utolewe, kuna pia hali tunayoifahamu huko Yemen, ” amesema rais wa Ufaransa.

Hivi karibuni viongozi wengi duniani wameishtumu Saudi Arabia baada ya kudhihirika kwamba mwandishi wa habari wa gazeti la Washington Post Jamal Khashogi, ambaye alikuwa mkosoaji mkubwa wa utawala wa kifalme nchini Saudia aliuawa katika ubaloi mdogo wa nchi hiyo nchini Uturuki.

Awali Saudi Arabia ilikanusha madai ya Uturuki kwamba mwandishi huyo aliuawa katika ubalozi wake mdogo mjini Istanbul.

Hata hivyo Rais wa Marekani Donald Trump anaendelea kuonyoshe uungwaji wake mkono kwaSaudi Arabia, licha ya kulaani mauaji dhidi ya mwandishi Jamal Kashoggi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.