Pata taarifa kuu
SYRIA-UN-USALAMA-HAKI

Syria yatakiwa kujieleza kuhusu wafungwa waliofariki gerezani

Tume ya Umoja wa Mataifa ya uchunguzi kuhusu uhalifu wa kivita nchini Syria imeitaka serikali ya Damascus kuzieleza familia za ndugu waliotoweka hatima ya ndugu zao na kuwakabidhi miili ya wale ambao waliuawa au walifariki kutokana na mateso waliopata gerezani.

Tume ya Umoja wa Mataifa ya Uchunguzi kuhusu uhalifu wa kivita nchini Syria, ikiongozwa na Paulo Pinheiro (kwenye picha).
Tume ya Umoja wa Mataifa ya Uchunguzi kuhusu uhalifu wa kivita nchini Syria, ikiongozwa na Paulo Pinheiro (kwenye picha). REUTERS/Denis Balibouse
Matangazo ya kibiashara

Ni vigumu kufikiria amani ya kudumu nchini Syria kama haki haitatendeka, tume hiyo imesema katika ripoti iliyowasilishwa kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.

Baada ya miaka kadhaa ya ukimya, mamlaka nchini Syria,mwaka huu ilitoa "maelfu au mamia ya maelfu" ya majina ya Wasyria ambao walifariki dunia kwa "sababu magonjwa" wakiwa kizuizini, kati ya mwaka 2011 na mwaka 2014.

"Vifo vingi pengine vilitokea katika maeneo ya yanayosimamiwa na Idara ya upelelezi au vitengo vya kijeshi. Tume ya Umoja wa Mataifa ya uchunguzi kuhusu uhalifu wa kivita nchini Syria haijaona serikali inakabidhi mwili wowote au baadhi ya vitu vya watu hao waliouawa," imesema taarifa .

Vyeti vingi vilivyotolewa kwa familia vinasema kuwa vifo vilitokea kutokana na "mshtuko wa moyo" au "infarctus," wamesema wataalam huru wa Umoja wa Mataifa chini ya uenyekiti wa Paulo Pinheiro kutka Brazil.

"Watu wengine kutoka mkoa huo tarehe zao za kufariki zinafanana,hali mabayo inaonesha kuwa kulikuepo na mauaji ya halaik," wataalamu hao wamongeza.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.