Pata taarifa kuu
ISRAEL-PALESTINA-USALAMA

Waziri wa Ulinzi wa Israel Avigdor Lieberman ajiuzulu

Waziri wa Ulinzi wa Israel Avigdor Lieberman amejiuzulu kwenye nafasi yake baada ya kutokubaliana kuhusu usitishwaji wa mapigano huko Gaza. Amebaini mbele ya waandishi wa habari kuwa mkataba wa kusitisha mapigano ni kama "kusalimu amri kwa ugaidi".

Waziri wa Ulinzi wa Israel Avigdor Lieberman Mei 18, 2018.
Waziri wa Ulinzi wa Israel Avigdor Lieberman Mei 18, 2018. Fuente: Reuters.
Matangazo ya kibiashara

Bw Lieberman amesema kufuatia hali hiyo chama chake cha mrengo wa kulia cha Yisrael Beiteinu kinaweza kujiondoa katika serikali ya mseto, hali ambayo inaweza kusababisha uchaguzi wa mapema.

Usitishwaji wa mapigano kwa kiasi kikubwa ulifanyika siku ya Jumatano, huku shule na shughuli za kibiashara kusini mwa Israel zikifunguliwa tena.

Mapema wiki hii wapiganaji wa Hamas na washirika wao walirusha usiku kucha roketi upande wa Israel, huku jeshi la Israel likiendelea na mashambulizi ya anga katika Ukanda wa Gaza.

Tangu Jumatatu alasiri, roketi 400 zilirushwa katika ardhi ya Israel kwa mujibu wa jeshi la Israeli, ambalo lilisema kwa ulipizaji kisasi, liliendesha mashambulizi dhidi ya ngome 150 za wapiganaji wa Hamas na mshirika wake, Islamic Jihad.

Mapigano hayo yalizuka baada ya miezi kadhaa ya mvutano. Wadadisi wanasema mapigano ambayo yangesababisha kuzuka kwa vita ya nne ndani ya miaka kumi kati ya Israel na Hamas ambayo inatawala bila kugawana madaraka na serikali ya Palestina katika Ukanda wa Gaza, eneo linalopatikana kati ya taifa la Wayahudi, Misri na bahari ya Mediterania.

 

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.