Pata taarifa kuu
PALESTINA-ISRAEL-USALAMA

Mapigano yaendelea kurindima Gaza

Wapiganaji wa Hamas na washirika wao wameendelea usiku kucha kurusha roketi upande wa Israel, huku jeshi la Israel likiendelea na mashambulizi ya anga katika Ukanda wa Gaza.

Ukanda wa Gaza waendelea kukumbwa na mashambulizi Novemba 12, 2018
Ukanda wa Gaza waendelea kukumbwa na mashambulizi Novemba 12, 2018 © AFP
Matangazo ya kibiashara

Haya ni mapigano makubwa tangu vita vya mwaka 2014 na huenda mapigano haya yakazua mgogoro mpya kati ya Palestina na Israel.

Tayari Wapalestina wanne wamepoteza maisha, kulingana na ripoti mpya, katika makabiliano hayo ambayo yamesababisha kifo cha mtu mmoja na wengine kadhaa kujeruhiwa nchini Israeli. Mtu huyo aliyeuawa nchini Israeli ni raia wa Palestina ambaye polisi wa Israel wamesema wanaendelea kuchunguza sababu za kuwepo kwake huko Ashkeloni.

Tangu Jumatatu alasiri, roketi 400 zimerushwa katika ardhi ya Israel kwa mujibu wa jeshi la Israeli, ambalo limesema kwa ulipizaji kisasi, limeendesha mashambulizi dhidi ya ngome 150 za wapiganaji wa Hamas na mshirika wake, Islamic Jihad.

Mapigano hayo yamezuka baada ya miezi kadhaa ya mvutano. Mapigano ambayo yanaweza kusababisha kuzuka kwa vita ya nne ndani ya miaka kumi kati ya Israel na Hamas ambayo inatawala bila kugawana madaraka na serikali ya Palestina katika Ukanda wa Gaza, eneo linalopatikana kati ya taifa la Wayahudi, Misri na bahari ya Mediterania.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.