Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 25/01 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 25/01 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 25/01 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Mashariki ya Kati

Yemen: Mattis atoa wito wa mazungumzo ya amani ndani ya siku 30

media Mji wa Sanaa, Oktoba 13, 2018. REUTERS/Mohamed al-Sayaghi/File Photo

Waziri wa Ulinzi wa Marekani ametoa wito kwa pande husika katika mgogoro nchini Yemen kusitisha vita na kuanzisha mazungumzo ya wazi ndani ya siku 30. James Mattis alikutana na viongozi kadhaa wa nchi za Kiarabu mwishoni mwa wiki iliyopitakando ya mkutano kuhusu usalama huko Bahrain.

Bw Mattis ana anaamini kwamba Saudi Arabia na Falme za Kiarabu wako tayari kuanza mazungumzo.

"Tunatoa wito kwa pande zote, waasi wa Houthi na muungano wa nchi za Kiarabu, kukutana nchini Sweden mnamo mwezi Novemba na kufikia suluhisho. Sio kujadili masuala yanayohusiana na masuala kama vile vile muda wa mazungumzo au idadi ya wajumbe wataokutana, " amesema James Mattis.

James Mattis ameongeza: "Mapigano yanapaswa kusitishwa, vita vinapaswa kurejelewa na maelewano. Ndani ya siku thelathini tunataka kuona pande zote zimeketi kwenye meza ya mazungumzo kwa lengo la kusitisha mapigano, kuondoa vizuizi kwenye mipaka, na kusitisha mashambulizi ya anga. Hali hiyo itamruhusu Mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa Martin Griffith kuzileta pamoja pande husika huko Sweden ili kukomesha vita hivi. Hii ndiyo njia pekee ya kutatua mgogoro huu. Tunapaswa kusonga mbele kwenye mchakato wa amani na hatuwezi kuahirisha jambo hili, tunapaswa kukamili hili ndani ya siku thelathini, vita hivi vimeendelea muda mrefu, na naamini kwamba Saudi Arabia na Falme za Kiarabu wako tayari. Na kwa hakika, kama waasi wa Houthi hawangelitojitoa kwenye mazungumzo ya mwisho yaliyoitishwa na Martin Griffith, tungekuwa tayari kwenye njia nzuri. "

Kwa upande wake, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Mike Pompeo siku ya Jumanne alitoa wito kwa muungano wa nchi za Kiarabu unaoongozwa na Saudi Arabia kusitisha mashambulizi ya anga nchini Yemen, huku akiwataka pia waasi wa Houthi kukomesha mashambulizi yao.

Vita vya Yemen ni kati ya vikosi vya serikali dhidi ya waasi wa Houthi, wakiungwa mkono na Iran, ambao mnamo mwaka 2014 na 2015 walivamia na kudhibiti maeneo makubwa ya nchi, ikiwa ni pamoja na mji mkuu Sanaa. Mnamo mwezi Machi 2015, muungano wa nchi za Kiarabu unaoongozwa na Saudi Arabia uliingilia kijeshi nchini Yemen kwa kuunga mkono majeshi ya serikali.

Mgogoro huu umeuawa watu 10,000, kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana